1.Mikakati ya wakereketwa wa udhibiti wa idadi ya watu barani Afrika
·Kile ambacho hawataki kusema:-
-Lugha yoyote inayoelekeza kwenye maana ya ‘‘mtoto’’ ‘‘haki ya kuishi’’ au ‘‘mtoto asiyezaliwa’’ haitamkwi.
-Baada ya kushindwa kuyatamka maneno hayo kwa sababu za kiitikadi sasa wanaweka maneno yenye kuficha maana yake halisi kama vile ‘‘kiumbe’’, ‘‘damu damu’’, ‘‘haki ya wanawake kuchagua’’ na ‘‘uchaguzi au uamuzi wangu’’.
-Wanakataa hoja zote za kimaadili na kuziita hoja hizo za kizamani, zimepitwa na wakati, hazina maana.
-Wanadai wanaishi maisha halisi na kuwa wanakwenda na wakati.
·Daktari Fred Sai, Rais wa IPPF, anasema, ‘‘utoaji mimba unaleta mkanganyiko mkubwa wa kimaadili duniani, ukijenga ukinzano kati ya wale wanaopendelea haki za wanawake kuua watoto wao kabla ya kuzaliwa na wale wanaoipinga haki hiyo’’. Wapo wale wanaodai kuwa mimba ni bonge la damu damu na wanamwona mwanamke kama chombo kitembeacho cha kumtunza mtoto kwa miezi tisa. Wapo wengine wanaohoji kuwa mimba ni mtoto mwenye kuwa na haki zake. Suala hili linakwenda nje ya utaalamu wa madawa na utendaji wa madaktari, lipo katika uwanja wa dini, maadili na falsafa.
Hatua saba za utekelezaji katika nchi zinazoendelea
1.Hulilenga bunge kwa hoja kuwa maendeleo ya kiuchumi yatapatikana kama watu watakuwa na familia ndogo.
·Hii ndiyo hali tuliyo nayo sasa katika nchi za Afrika Kusini mwa Sahara
·Bunge linatunga sheria za kuruhusu matumizi ya vidhibiti mimba, na kuondoa vikwazo vinavyozuia upatakanaji na utumiaji wake.
2.Sambaza vidhibiti mimba nchini kote kwa lugha laghai za ‘‘wataalamu wa uzazi wa mpango’’.
·Sema tunatekeleza programu za ‘‘afya ya kizazi’’, ‘‘afya ya ujinsia’’, ‘‘kupanga uzazi’’
·Tumia jina na mifumo ya Wizara ya Afya ili kupata ukubalifu na mafanikio
·Anzisha kliniki binafsi na tekeleza malengo fichika (Marie Stopes).
·Tengeneza mfumo wa ‘‘wasambazaji msingi’’ wanaoweza kwenda nyumba kwa nyumba.
3.Ishawishi serikali kulipia na kuendesha kwa nguvu programu na propaganda ya uzazi wa mpango ‘‘kwa njia za kisasa’’.
·Hali hiyo inafungua milango kwa uwezekano wa kutunga sheria ya kutoa mimba.
·Utoaji mimba usio salama unajenga hitaji la kuwa na huduma za uzazi wa mpango
·‘‘Usio salama’’ maana yake ‘‘usiohalalishwa’’ na hivyo kutoa shinikizo la kuhalalisha utoaji mimba
4.Tumia mtandao wa kliniki za serikali na makundi ya uzazi wa mpango kuanzisha programu za kuwafunga watu kizazi, hasa wanawake maskini sana (tumeona mfano wa programu hii kule mwambao wa ziwa Nyasa, vijiji vya Mbamba Bay hadi Chiwindi mpakani na Msumbiji)
·Lengo ni kuona kuwa watu hawazai kabisa
5.Pigania kutungwa sheria za kutoa mimba (kuua watoto kabla ya kuzaliwa)
·Kwa sasa ni njia ya kukabiliana na mimba zisizopangwa (zisizotarajiwa).
·Ni njia muhimu inayotumika baada ya kushindwa vidhibiti mimba, yaani mwanamke amepata mimba licha ya kutumia vidhibiti mimba.
·Kukubali utoaji mimba kwa masharti Fulani.
·Baada ya kuhalalisha utoaji mimba masharti yote huondolewa
·Kumbuka lengo la watoaji mimba, wadhibiti idadi ya watu na watumiao vidhibiti mimba hufurahia kuona mizoga ya watoto.
6.Tumia programu za uzazi wa mpango na elimu ya [familia] ngono kufikia malengo hayo
7.Gundua au tia chonjo kwa tatizo fulani la kijamii linalopelekea haja ya programu na huduma za matumizi ya vidhibiti mimba.
·UKIMWI ni moja ya hali hizo ambayo inajenga utegemezi katika matumizi ya kondomu
·Sema kuwa kondomu ni zana muhimu katika kuzuia maambukizo ya virusi vya UKIMWI, sheria zitungwe kuondoa vikwazo dhidi ya matumizi yake
·Tumia vyombo vya habari kuhamasisha na kujenga ukubalifu wa kondomu
2.Mkakati wa Afrika
Hatua saba kwa kadiri ya maneno na machapisho ya wadhibiti idadi ya watu
a)Wanalenga serikali kwa wito kuwa familia ndogo huleta maendeleo
·Kamati ya Ushauri ya Afrika juu ya Masuala ya Idadi ya Watu (African Population Advisory Committee) iliundwa April, 1989
·Miaka ya mwanzo ya mwongo wa 1980, ilikadiriwa kuwa asilimia 60 ya serikali za Afrika ziliridhika na ukuaji wa idadi ya watu katika nchi zao.
·Ni nchi tatu zilikuwa na sera ya idadi ya watu Kenya, Ghana na Mauritus. Mtazamo ulioenea kuwa shinikizo la kupunguza ukuaji wa idadi ya watu kutoka nchi fadhili za Magharibi ulifanya masuala ya idadi ya watu na uzazi wa mpango kuwa ni masuala nyeti kisiasa. Ukuaji wa idadi ya watu haukupewa kupaumbele. Katika muda wa miaka kumi iliyofuata palitokea mabadiliko makubwa katika mitazamo ya serikali mbalimbali. Kwa kadiri matatizo yaliyohusiana na ukuaji wa idadi ya watu na maendeleo ya kijamii na kiuchumi yalivyoibuka na ndivyo hivyo zilivyotungwa sera kitaifa za idadi ya watu katika nchi mbalimbali. Kufika mwishoni mwa mwongo huo serikali nyingi zilibaini kuwa ongezeko la watu katika nchi zao lilikuwa kubwa mno.
b)Jaza nchi wataalamu wa uzazi wa mpango na vidhibiti mimba
·USAID ilitoa $ 81.4 milioni kwa nchi kumi za Afrika kwa ajili ya huduma za afya ya kizazi mnamo 1999.
·USAID ilitoa $ 22.4 milioni kwa Tanzania mnamo 2003.
Msaada wa UNFPA kwa Tanzania kwa miaka mitano ijayo (2002-2007) ni $ 28.25 milioni.
c)Ishawishi serikali ILIPIE na kuhamasisha vifaa hivi vya kifo
·Matashi ya kisiasa na uongozi bora ni muhimu ili kuhalalisha na kurahisisha kukubalika kwa programu za kitaifa za uzazi wa mpango. Matashi haya ya kisiasa yanaonekana katika vitendo halisi vinavyowezesha programu kupanuka, kama vile kuongeza fedha katika programu hizo, kuondoa vizuizi vya kisheria na kutunga sheria zinazoondoa vizuizi, na kuanzisha miundo mbinu inayoonyesha wajibu wa kila sekta na mahusiano.
·Kenya ni mfano mzuri wa serikali iliyodhamiria kuendeleza uzazi wa mpango. Mnamo 1982 serikali ya Kenya iliweka masuala ya udhibiti wa idadi ya watu katika chombo kipya ‘‘National Council Population and Development’’ chini ya ofisi ya makamu wa Rais. Kufikia 1984 matashi ya serikali ya kupunguza ongezeko la watu yalifikia upeo. Serikali iliondoa ushuru wa kodi za mauzo kwa vidhibiti mimba na kuanzisha programu za semina kwa viongozi katika masuala ya udhibiti wa idadi ya watu na haja ya kuwa na familia ndogo. Katika semina ya kwanza Rais Moi aliongea juu ya haja ya kupanua huduma za uzazi wa mpango, alitoa wito kwa viongozi wa kitaifa na vijiji kuunga mkono programu hiyo na alitangaza kuweka shughuli hizo katika ngazi ya serikali za mitaa na wilaya . Huo ukawa mwanzo wa programu kubwa ya uzazi wa mpango nchini Kenya. Serikali, asasi zisizo za kiserikali na wafadhili walizidisha juhudi katika kutoa huduma bora kupitia miundo mbinu mipya na uingizaji wa njia za uzazi wa mpango. Malengo ya muda mrefu ya Kenya katika miaka ya 1990 yalihusu kupunguza ukuaji wa idadi ya watu kutoka asilimia 3.6 kwa mwaka hadi asilia 2.5 kufikia mwaka 2000 na kuongeza matumizi ya vidhibiti mimba kutoka asilimia 27 hadi 30 kufikia 1995 na asilimia 40 kufikia mwishoni mwa mwongo huo.
d)Tia chonjo kwa tatizo la kijamii ili kujenga hitaji la uzazi wa mpango
·Mnamo 1994 kulifanyika kongamano juu ya utoaji mimba usio salama huko Mauritius
·Jitihada za kujenga hofu kwa serikali za Kiafrika juu ya ukuaji wa idadi ya watu na kukua umaskini.
·Mbinu: unganisha makundi yote yanayoshughulika na udhibiti wa idadi ya watu na kujenga mkakati wa pamoja ili kutafuta mamilioni ya dola kwa ajili ya programu za uzazi wa mpango.
·Hatimaye kuhusisha suala la utoaji mimba usio salama na hitaji la huduma za uzazi wa mpango baada ya kutoka mimba (hapa Tanzania huduma hiyo huitwa ‘‘Post Abortion Care’’ na vifaa vitumikavyo kwa huduma hiyo huitwa Manual Vacuum Aspirators - MVA; ambavyo baadhi ya kliniki hutumia kwa kutoa mimba kati ya mwezi mmoja hadi mitatu).
·Kueneza huduma za kufunga kizazi kama ilivyokuwa katika kongamano la mwaka 1994. Huduma hizo hutolewa kwa kivuli cha ‘‘afya ya ujinsia’’ na ‘‘afya ya kizazi’’ kwa wanaume na wanawake na ‘‘huduma za kizazi’’ kwa wanawake.
e)Pigania uhalalishaji wa utoaji mimba
·Hapa ni jinsi wapiganiaji kifo wanavyofikiri kuhusu sheria zinazowalinda watoto dhidi ya kuuawa.
·Sheria za utoaji mimba hapa Afrika zinatokana na sheria za kikoloni kama vilevile ile ya Kingereza kuhusu SHERIA YA BINADAMU ya mwaka 1920: nchi zenye kufuata sheria hizi huzuia utoaji mimba kwa hali yoyote ile. Baadhi ya nchi kama vile Ghana na Zambia zimerekebisha sheria hizi ili kuruhusu utoaji mimba katika mazingira fulani, kama vile hatari kwa afya ya mama, matatizo ya tumbo la kizazi, mimba ya ndugu, mzazi/mtoto/ au mimba ya kubakwa au hata matatizo ya kijamii na kitabibu. Hakuna sheria iliyovuka mpaka kama vile ile ya Afrika Kusini inayoruhusu utoaji mimba hata kama hakuna sababu yoyote.
·Utoaji mimba utaruhusiwa hatua kwa hatua hadi pale vizuizi vyote vitakapokuwa vimeondolewa kufanya utoaji mimba kuwa jambo la kawaida katika jamii.
·Hoja kama utoaji mimba uruhusiwe au usiruhusiwe usitegemee suala kuwa mimba ina uhai au roho au hapana. Kulaani utoaji mimba kunatokana na sababu za kimaadili tu ni kushindwa kutambua, kukabili na kushughulikia masuala yatukabiliyo.
f)Afrika ya Kusini ni mfano wa nchi ambamo vizuizi vyote dhidi ya utoaji mimba vimeondolewa,
·Siyo tu kwamba mimba inaweza kutolewa wakati wowote ule, imewekwa kisheria kuwa kosa kumzuia mwanamke aliyeamua kumwua mtoto wake.
Sheria imeweka adhabu ya $ 22,000 na kifungo cha miaka 10 kwa kosa la kumzuia mwanamke kumwua mtoto wake.