With much of the world ravaged by global conflicts belonging to what Pope Francis has dubbed al a “third world war fought piecemeal,” an international association dedicated to promoting peace and...
“From the beginning, I spoke of a plot against me: An investigation built on falsehoods, which five years ago unjustly devastated my life and exposed me to a pillory of global proportions,” Cardinal...
On Monday the Peru-based Sodalitium Christiane Vitae (SCV) announced its formal suppression, bringing to an end a decade-long saga.
Utangulizi
Siku hizi utoaji mimba unaelekea kuwa utamaduni wa wanawake wengi duniani, hapa kwetu Tanzania vilevile. Jambo la kutoa mimba limekuwa la kawaida sana na inaelekea jamii imeanza kulizoea na kuliona kuwa ni tukio la kawaida. Ni kama vile halina madhara makubwa.
Leo tunaanza kujadili mada inayohusu LAANA itokanayo na utoaji mimba.
Hebu kwanza tuangalie maana ya laana: kwa kadiri ya “Concise Oxford English Dictionary”, Oxford University Press, 2002, neno “curse” limetafsiriwa kama,
A solemn appeal to a supernatural power to inflict harm on someone or something => a cause of harm or misery
An offensive word or phrase used to express anger or annoyance
Katika maana hizo mbili, sisi tutachukua ile maana ya kwanza, yaani laana kama kisababishi cha madhara au maumivu au huzuni au mateso.
Laana ya utoaji mimba inatokana na ukiukaji wa amri ya Mungu ‘USIUE’ (Kut. 20:13). Uuaji ni kosa linalokwenda kinyume na matashi ya binadamu ya kuheshimu na kulinda uhai wa binadamu. Hata katika sheria za nchi mbalimbali zinaweka adhabu kali kwa kosa la binadamu kumwua binadamu mwingine. Na anayemwua mwingine katika dhamiri yake anaisikia ile laana ya Mungu ikitamkwa waziwazi ‘UMELAANIWA WEWE’ na baada ya hapo anakabiliwa na adhabu zinazomsabishia mateso/maumivu/majuto/huzuni.
Laana ya utoaji mimba inajitokeza katika maumbo na matendo mabalimbali na kwa watu mbalimbali. Iko laana anayoipata mwanamke mtoaji mimba; iko laana inayowapata watoto wanaosalimika katika jaribio la kutoa mimba au waliozaliwa kabla au baada ya mwenzao kuuawa, au watoto waliozaliwa katika nchi ambayo imepitisha sheria ya utoaji mimba. Vilevile iko laana inayompata daktari au mtu yeyote aliyemwua huyo mtoto kabla hajazaliwa. Tutatazama vilevile jinsi laana ya utoaji mimba inavyozikumba familia. Tutajadili pia laana ya utoaji mimba ambayo imetapakaa katika jamii yetu ya leo.
Laana kwa mwanamke aliyetoa mimba
Hebu tuiangalie kwanza laana katika muktadha ya Biblia Takatifu ili tuone jinsi inavyohusiana na laana ya utoaji mimba katika enzi zetu. Laana hutolewa/hutamkwa na Mungu baada ya mwanadamu kukiuka amri zake au maagizo yake. Daima laana inaambatana na adhabu ambayo yaweza kuwa ya kimwili, kisaikolojia au kiroho
“Kaini akamwambia Habili nduguye, ‘Twende uwandani”. Ikawa walipokuwapo uwandani, Kaini akamwinukia Habili nduguye, AKAMWUA. Bwana akamwambia Kaini, “Yuko wapi Habili ndugu yako?” Akasema, “Sijui, mimi ni mlinzi wa ndugu yangu?” Akasema, “Umefanya nini? Sauti ya damu ya ndugu yako inanililia kutoka katika ardhi! Basi sasa UMELAANIWA wewe katika ardhi, iliyofumbua kinywa chake ipokee damu ya ndugu yako kwa mkono wako; utakapoilima ardhi haitakupa mazao yake; utakuwa mtoro na mtu asiye na kikao duniani” (Mwa.4:8-12).
Katika kisa hiki, Kaini analaaniwa na Mungu baada ya kutenda kosa kubwa, yaani la kumwua nduguye Abel. Laana ya Mungu kwa Kaini inaambatana na adhabu ambayo ndiyo inakuwa kisababishi cha mateso yaliyomkabili Kaini.
Laana hii ya Kaini inafanana kwa uzito wake na laana ile aliyotoa Mungu kwa nyoka.
“Bwana Mungu akamwambia nyoka, ‘Kwa sababu umefanya hayo, umelaaniwa wewe kuliko wanyama wote, na kuliko hayawani wote walioko mwituni; kwa tumbo utakwenda, na mavumbi utakula siku zote za maisha yako; nami nitaweka uadui kati yako na huyo mwanamke, na kati ya uzao wako na uzao wake; huo utakuponda kichwa, na wewe utamponda kisigino” (Mwa.3:14-15).
Nyoka au Ibilisi/Shetani analaaniwa kwa kupingana na amri ya Mungu kwa kusababisha mwadamu akiuke maagizo yake Mungu. Mungu anatamka kwanza laana yenyewe na kisha adhabu inayomsababishia nyoka maumivu/uchungu/mateso.
Laana ya kwanza
Laana inayomkabili mwanamke anayemwua mtoto wake kabla hajazaliwa. Kuna baadhi ya wanazuoni wanagawa laana hiyo katika makundi ya muda mfupi na muda mrefu. Hebu tuangalie laana hiyo katika mtazamo wa kisa cha Kaini na Abel.
Kwa kumwua mtoto wake mwanamke anatoa kafara ya mtoto wake na damu yake kuwa chakula cha Ibilisi. Mungu anamwambia Kaini ‘damu ya ndugu yako inanililia kutoka katika ardhi’. Kumbe damu ya mtoto anayeuawa inamwagika ardhini na maiti ya mtoto aliyeuawa inatupwa ardhini na hivyo kuwa ndicho chakula cha Ibilisi. Kwa kadiri idadi ya wanawake watoaji mimba inavyoongezeka ndivyo hivyo Ibilisi anavyojipatia chakula chake kwa wingi. Tukumbuke daima kuwa katika kila tendo la utoaji mimba, mwanamke anamwaga damu yake na mtoto sio tu anamwaga damu bali pia mwili wake. Kwa hiyo Ibilisi anajilisha kwa damu itokayo kwa mama wa mtoto, damu na maiti ya mtoto aliyeuawa katika kitendo cha utoaji mimba. Na Ibilisi anachochea sababu au visingizio vingi kwa wanawake kuwaua watoto wao. Kilele cha ushindi wa Ibilisi ni pale nchi inapofikia hatua ya kutunga sheria za kuwaua watoto kabla ya kuzaliwa.Na pengine Ibilisi anahusisha vitendo hivyo vya kikatili dhidi ya watoto na vuguvugu la wanawake kudai haki zao; wakisema kuwa wana haki juu ya miili yao au ni uhuru wa uchaguzi. Vilevile Ibilisi amempatia binadamu maneno na lugha tamu ili kuhalalisha vitendo hivyo viovu – haki ya afya ya kizazi, uzazi wa mpango. Hayo yanafanyika ili kujenga uhalali wa binadamu kuvikubali vitendo ambavyo kwa asili yake ni viovu. Ndivyo hivyo Ibilisi anavyofanya ili kujipatia mawindo yake. Kwa hiyo kuna uhusiano mkubwa kati ya utoaji mimba na nguvu za kishetani zinazochochea vitendo hivyo.
Laana ya pili
Vitendo vya utoajimimba vinahusisha matumizi ya nguvu katika kupanua shingo ya kizazi ambayo baada ya kupata uja-uzito ilifunga ili kumlinda mtoto hadi siku ya kujifungua. Matumizi haya ya nguvu yanayohusisha vifaa visivyo na vionjo hufanya shingo ya kizazi kulazimika kufunguka na hivyo, kwa vile hiki ni kitendo kilicho kinyume na utaratibu wa nguvu za maumbile, basi shingo ya kizazi hulegea na haitafungika tena kufikia ukamilifu wake. Hali hiyo inasababisha mimba zinazofuatia kutoka zenyewe. Ni balaa iliyoje kuona watoto wanaofuatia baada ya mwenzao kuuawa wanachopoka wenyewe kutoka tumboni kutokana na kulegea na uharibifu wa viungo vya kizazi. Huu ndio mwendelezo wa laana kufuatia laana ya kumwua mtoto asiyekuwa na hatia na ambaye hana nguvu ya kujitetea.
Laana ya tatu
Utoaji mimba unahusisha kuingizwa katika viungo vya kizazi vifaa ambavyo havijali ubinadamu wa mtu. Vifaa hivyo vinavyoingizwa kwa nguvu kwa kusukuma na kuvuta huweza kusababisha michubuko na majeraha katika viungo vya kizazi na hivyo kuwa na uwezekano mkubwa wa kupata donda ndugu, yaani majeraha yasiyopona na hii ndiyo saratani ya shingo ya kizazi. Lakini pia wakati mimba imetungwa mama huanza kuandaa maziwa katika matiti yake kwa ajili ya kumnyonyesha mtoto. Kama uhai wa mtoto umekatishwa ghafla, maziwa huharibika na kutengeneza sumu ambayo inashambulia ya matiti ya mama na hivyo kusababisha saratani ya matiti. Mwanamke aliyepata saratani kama hajapata matibabu ya mapema anaendelea kuteseka kadi kifo chake. Baadhi ya tiba huhusisha kukata matiti ili kusalimisha uhai wa mama. Kwa vyovyote vile, hakuna daktari anayeweza kukata shingo ya kizazi, na hali hiyo husababisha vifo kwa wanawake wengi.
Laana ya nne
Yawezekana vitendo vya utoaji mimba vikaharibu mfumo wa uzazi, au kwa kuchana mfuko wa kizazi na hivyo kulazimika kuutoa wote na hivyo mwanamke huyo hawezi tena kupata uja-uzito. Katika vitendo vya utoaji mimba yawezekana mwanamke akavuja damu nyingi hadi kifo; au pengine katika utoaji mimba mishipa ya fahamu ikaharibiwa na hivyo kumsababishia mwanamke kifo chake. Kwa kifupi tunaweza kusema kuwa mwanamke anayetoa mimba anakabiliwa na laana mbili kwa mara moja, laana ya kutozaa tena na laana ya kifo chake mwenyewe.
LAANA YA UTOAJI MIMBA
Jambo la kutoa mimba limekuwa la kawaida sana na inaelekea jamii imeanza kulizoea na kuliona kuwa ni tukio la kawaida. Ni kama vile halina madhara makubwa.
Msikilizaji mmoja wa Kipindi chetu cha Radio Maria kutoka Uingereza alituuliza, kwa nini tunatumia dhana ya laana badala ya madhara. Na akashauri kuwa ingefaa tuendelee kutumia dhana ya madhara badala ya laana. Tulimjibu kuwa hoja zetu zinatokana na misingi ya Ki-Biblia ambapo tunashuhudia Mungu akitamka kwanza laana na kisha anatoa adhabu. Ili tufahamu vizuri zaidi dhana hiyo, hebu kwanza tuangalie maana ya laana: kwa kadiri ya “Concise Oxford English Dictionary”, Oxford University Press, 2002, neno “curse” yaani ‘laana’ kwa Kiswahili, limetafsiriwa kama,
A solemn appeal to a supernatural power to inflict harm on someone or something => a cause of harm or misery
An offensive word or phrase used to express anger or annoyance
Katika maana hizo mbili, sisi mechukua ile maana ya kwanza, yaani kisababishi cha madhara au maumivu au huzuni au mateso.
Laana ya utoaji mimba ni ukiukaji wa amri ya Mungu ‘USIUE’ (Kut. 20:13). Uuaji ni kosa linalokwenda kinyume na silika na matashi ya binadamu ya kuheshimu na kulinda uhai wa binadamu. Maumbile ya u-binadamu wetu yanakataza mtu kumwua mwenzake. Hata katika sheria za nchi mbalimbali zinaweka adhabu kali kwa kosa la binadamu kumwua binadamu mwingine. Mungu aliongea na mababu zetukama vile Ibrahim na Musa, ana kwa ana. Leo hii baada ya kupokea amri za Mungu na kustawishwa na Kristo kwa neema zake, binadamu anaongea na Mungu kwa njia ya dhamiri. Dhamiri zetu zinatuelekeza kutenda mambo mena na kuepa mabaya. Na baada ya kumwua mtoto kabla ya kuzaliwa mwanamke anaisikia ile laana ya Mungu ikitamkwa waziwazi ‘UMELAANIWA WEWE’ na baada ya hapo anakabiliwa na adhabu zinazomsabishia mateso/maumivu/majuto/huzuni.
Tunajadili mada ya madhara yatokanayo na utoaji mimba kwa mwanamke kwa kuzingatia kipengele cha laana ya kisaikolojia. Katika kujadili mada hiyo tunanze kwa kutafakari kisa cha kweli kilichomsibu mwanadada mmoja wa Marekani, aitwaye Tracy Black ambaye alitoa mimba ya miezi miwili kama nilivyokisoma katika kitabu, “…and still they weep: personal stories of abortion”, kilichoandikwa na Melanie Symonds, na kuchapishwa na The SPUC Educational Research Trust, 1996. Katika kitabu hiki wanawake wengi wametoa shuhuda zao.
Tracy Black alizaliwa na kulelewa katika familia ya wazazi wacha Mungu. Wazazi hawa hawakupenda watoto wao waingie kwenye ndoa wakiwa na watoto kabla ya ndoa. Akiwa amefikisha miaka 19, Tracy tayari alikuwa na kazi ya ajira katika chuo kikuu kimoja na alikuwa na mpenzi wake aliyejulikana kama Scott. Baada ya ya miezi sita ya uhusiano wao kimapenzi, Tracy aligundua kuwa alikuwa na uja-uzito wa miezi miwili. Kwa kuogopa kusemwa na wazazi, aliamua kutoa mimba ile kwa kutumia vidonge vya kutolea mimba viitwavyo RU486. Siku mbili baada ya kumeza vidonge hivyo alirudi katika kliniki na kufanyiwa usafishaji ambapo aligundua kuwa mimba yake ilikuwa imetoka. Tracy anasimulia kuwa alipata maumivu makali sana baada ya kumeza vidonge hivyo na wakati wa kusafishwa, lakini anasema maumivu aliyoyapata baada ya kutoa mimba yalikuwa makubwa zaidi. Mwezi mmoja baada ya kitendo cha kumwua mtoto wake, Tracy alijikuta akikabiliwa na matatizo yafuatayo:
alikuwa akijichunguza kila siku usiku,
alikuwa hawezi kwenda nje na alikuwa akiogopa kwenda sehemu za wazi, hali inayojulikana kwa kiingereza kama “agoraphobic”.
alijikuta akiwaogopa mbwa kana kwamba walikuwa wanamwambukiza vidudu vya magonjwa
Alipomwona daktari aliambiwa kuwa hali hiyo ilitokana na msongo wa mawazo. Hata jitihada za kumpatia dawa za kuondoa maumivu hazikufaa kitu. Tracy hakuweza tena kufanya kazi kwa kiwango kilichotakiwa. Alipomwona mshauri nasaha aliambiwa kuwa alikuwa na hali ya ugonjwa ijulikanayo kama ‘msukumo wa hali ya juu wa kukosa utaratibu katika maisha’.
Matatizo mengine aliyoyapata ni pamoja na
tabia aya kuhesabu vitu vilivyopo [kila kimoja kilihesabiwa],
kufanya usafi uliovuka mipaka hasa wa vyombo vya jikoni,
alikuwa anakula sana chokoleti
mara nyingi alijisikia mkosaji
Kitulizo chake ni mtoto wa dada yake Darren ambaye alichukuliwa kama mbadala wa mtoto wake aliyemwua. Darren ni mkubwa na anapishana na mtoto wake kwa mwezi mmoja.
Mbaya zaidi Tracy alikuwa na mawazo ya kufanya vitendo viovu na kuwa na usongo mkubwa wa mawazo
Tuitazame laana iliyomsibu mwanadada Debbie kama kilivyosiliwa katika kijitabu “Beyond Choice”, kilichoandikwa na Don Baker na kuchapishwa na Multnomah Press, Portland, Oregon, 1985
Debbie alipata uja-uzito ambao haukuwa na matarajio baada ya tendo moja tu la ngono akiwa sekondari. Baada ya uja-uzito huo Debbie alijisikia mnyonge, na alikuwa hatoki nje ya chumba chake na hata chakula alikuwa akipelekewa huko. Siku moja mama yake alimchukua Debbie na kumpeleka kwenye kituo cha kutolea mimba na kulipia dola za Kimarekani 225. Baada ya kutoa mimba hiyo Debbie na Tim, mshikaji wake walitoroka nyumbani na kwenda kujitegemea. Wakiwa huko Debbie alianza kutumia huduma za uzazi wa mpango, lakini hata hivyo alipata mimba tena na kuitoa baada ya kugundua kuwa mshikaji wake alimtelekeza, hakuwa na fedha za kujihudumia na kumhudumia mtoto, umri wake ulikuwa bado mdogo. Debbie alirudi kwa wazazi wake na alirudi shuleni kumaliza masomo yake, lakini tayari alikuwa amepondeka na kujeruhiwa. Baada ya hapo Debbie alibadilisha wavulana akapata mimba baada ya nyingine na zote alizitoa. Hakuweza kudumu katika kazi ya ajira kutokana na msongo wa mawazo kutokana na kufukuzwa na wanaume aliokuwa na kimapenzi na waliompatia mimba. Wakati wa maisha yake Debbie alijisikia mpweke, baada ya kukosa mtu wa kumfariji, alitumia muda mwingi katika kulia. Alipotakiwa na mshauri nasaha kueleza jinsi anavyojisikia, Debbie alisema
Alijiona ametenda dhambi ya kuua
Alijisikia kutengwa
Alijiona mwenye hasira/maumivu makali
Alijisikia mkosaji
Alijiona mtu asiyekuwa na lengo la maisha
Maisha ya Debbie yalirudi katika hali ya kawaida baada ya kupokea ushauri nasaha na uponyaji. Katika uponyaji Debbie alitakiwa kukiri na kutamka waziwazi yafuatayo; “Mpendwa Bwana Yesu, najua kuwa mimi ni mdhambi na nahitaji msamaha wako. Naamini kuwa ulikufa kwa ajili ya dhambi zangu. Nataka kuziacha dhambi zangu. Nakualika sasa uje moyoni na katika maisha yangu. Nataka nikuamini wewe tu kama Mwokozi na kukufuata kama Bwana, katika ushirika wa kanisa lako”
Baada ya sala hiyo Debbie alilia kimyakimya, mwenye amani tele na mwenye shukrani kuu. Na usiku alipata usingizi mzuri na wenye amani. Debbie alipata mchumba Steve na wakafunga ndoa na kuishi maisha ya amani.
Tumalizie mada yetu kwa kisa kingine ambacho kinasimuliwa katika kijitabu, “Mama! Why did you kill Us?”, kilichoandikwa na Domenico Mondrone na kupigwa chapa na Tan Books and Publishers, Inc. Rockford, Illinois.
Kijitabu hiki kinasimulia kisa cha mwanamama aliyetoa mimba saba na baada ya vitendo hivyo alipata nini?
Kwikwi, wasiwasi
Kilio, huzuni na kujikatalia
Kukosa amani na utulivu
Hali ya hofu na maumivu
Usiku mmoja akiwa amelala, mama huyu alisikia sauti ya mtoto mchanga ikiita ‘MAMA’ lakini hakujua ilitoka wapi sauti hiyo. Baada ya robo saa alisikia sauti za watoto wengi zikiita ‘MAMA’ na tena baada ya muda ziliita tena ‘MAMA’ tena kutoka umbali wa karibu sana.
Mama huyu alijiuliza, jee haya ni mashetani? Alifikiri labda alikuwa anaanza kupata dalili za wenda wazimu.
Alijikakamua akauliza, ‘lakini ni nani anayeniita”? Wale watoto wakamjibu; ‘ni sisi ‘MAMA’.
Akauliza tena na ninyi ni nani? Wakamjibu, ‘ni sisi watoto wako ambao hukuturuhusu tuzaliwe’
Mama huyu akaishiwa nguvu. Na akawasikia tena wakimwambia, ‘tazama wote saba tuko hapa pamoja nawe’.
Baada ya pale aliona vivuli vya watoto saba vikitembea kati yake na ukuta na vikiwa vinabadilishabadilisha umbile. Akajiuliza, jee nimekuwa kichaa? Wale watoto wakamjibu, ‘hapana, wewe si kichaa, unachokiona ni ukweli mtupu. Unajisikia tu mkosaji baada ya kutuua tukiwa tumboni mwako. Sisi sio vivuli, bali watoto halisi. Kama unataka ukweli tutakudhihirishia jambo hilo. Masaa machache yaliyopita baba yetu amekufa lakini hayuko nasi’. Yule mama alisimia jinsi wale watoto walivyomwangalia kisha wakatoweka.
Mama huyu alirudia hali yake baada ya kupata ushauri nasaha na uponyaji.
Baada ya kujadili laana zilizowasibu akina mama hao watatu, wataalamu wa saikolojia wamefanya majumuisho katika kuangalia laana za kisaikolojia zinazowapata wanawake baada ya kuwaua watoto wao kabla ya kuzaliwa kama:
kujihisi mkosaji,
kujihisi mwuaji,
·kujihisi umepotelewa na kitu fulani maishani,
·kulia na kujutia,
·kuhangaika na kukosa amani,
·kuweweseka na maono,
·kupoteza uwezo wa kufanya maamuzi,
·kutawaliwa na mawazo ya kifo,
·kujenga tabia ya ukatili,
·kukabiliwa na hasira,
·kukata tamaa,
·kujihisi umepoteza hali na haki ya umama,
·kuwatamani na kuwapenda watoto wa wengine,
·kutamani kuvunja mapenzi,
·kukosa uwezo wa kusamehe,
·kujihisi kunyonywa
Kila mwaname aliyeshiriki vitendo vya utoaji mimba hupata laana hizo, yaweza kuwa moja, mbili, tatu au hata nne ana zaidi. Tukumbuke tulivyosema mwanzoni, Mungu hutamka laana kwa njia ya ndamiri zetu na laana hizo hufuatiwa na adhabu ambazo nyingine zaweza kudumu katika maisha yote ya mhusika.
LAANA YA UTOAJI MIMBA
Jambo la kutoa mimba limekuwa la kawaida sana na inaelekea jamii imeanza kulizoea na kuliona kuwa ni tukio la kawaida. Ni kama vile halina madhara makubwa.
Lakini baada ya kusikiliza mifano ya laana kutoka kwa wanawake kadhaa wa huko Marekani waliowahi kutoa mimba, ndipo ukweli wa laana utokanao na utoaji mimba ulipofunguka. Tulisema katika kuhitimisha mada yetu kuwa wanawake wanapata laana za aina mbalimbali kama vile;
kujihisi mkosaji,
kujihisi mwuaji,
·kujihisi umepotelewa na kitu fulani maishani,
·kulia na kujutia,
·kuhangaika na kukosa amani,
·kuweweseka na maono,
·kupoteza uwezo wa kufanya maamuzi,
·kutawaliwa na mawazo ya kifo,
·kujenga tabia ya ukatili,
·kukabiliwa na hasira,
·kukata tamaa,
·kujihisi umepoteza hali na haki ya umama,
·kuwatamani na kuwapenda watoto wa wengine,
·kutamani kuvunja mapenzi,
·kukosa uwezo wa kusamehe,
·kujihisi kunyonywa
Leo tunaendelea na mada hiyo, na bado tunaangalia laana wazipatazo wanawake waliotoa mimba. Baada ya kipindi cha juma lililopita nilipata simu nyingi zikiniuliza, “na wanaume je waliohusika na mimba hizo, nao wanapata laana”? Hatutajibu swali hilo leo, bali tutafanya hivyo jumala lijalo. Kwa leo bado tunaendelea kusikiliza shuhuda zinazotolewa na wanawake watesekeo baada ya kutoa mimba. Tusikie kisa cha Bernadetta Thompson wa Uingereza.
Bernadetta anaanza kutoa ushuhuda ifuatavyo:
Miaka mingi ya nyuma nilizoea kujificha lizungumzwapo suala la utoaji mimba hasa katika vyombo vya habari. Lakini tangu hapo nimepitia vipindi mbalimbali vya uponyaji. Hata baada ya miaka 21 ya uponyaji bado majeraha yaliyoachwa na vitendo vyangu vya utoaji mimba hayajapona na yananifanya nitende kama miaka ile ya kujikatalia. Hali hiyo ilijitokeza hivi karibuni baada ya mpwa wangu kujifungua nami nilishindwa kwenda kumwona hospitalini alikolazwa na hata baada ya kujifungua kwani nilijisikia aibukwenda kumwoma mtoto. Nilipojitutumua kwenda nilibubujikwa na machozi nilipomshika mtoto Joel mikononi mwangu. Nilikumbuka kuwa umri wa mama yake ulikuwa sawasawa na umri wangu nilipotoa mimba yangu na fikra hizo ziliibua hisia kali ndani yangu
Miaka ya nyuma nilishindwa kuwaambia wazazi wangu kuwa nilikuwa mja-mzito, na kwamba ilikuwa imetoka yenyewe tu (miscarriage) kwani nilikuwa nimepata mchumba katika kipindi ambacho mimba yangu ilikuwa imeharibika. Kwa bahati mbaya sikupata nafasi ya kuomboleza. Nilitegemea kupata mtoto mwenye afya kutoka kwa mchumba wangu. Nilizoea kushika tumbo langu lenye mtoto nikiwa bafuni na kuongea naye nikimweleza kuwa mimi ndiye mama yake. Mchumba wangu aliponitembelea siku moja hakuwa na jambo jingine bali kunieleza kuwa lazima nitoe mimba hiyo. Nilihuzunika sana, kwani wazo tu la kutoa mimba lilimaanisha mchumba wangu alidhihirisha katao sio tu kwa mtoto bali kwangu pia. Sikuelewa kwa nini mchumba wangu aliniambia nitoe mimba ambaye ni mtoto wetu. Lakini matamshi yake yakawa yamepanda mbegu mbaya katika akili yangu iliyokuwa imechanganyikiwa wakati huo.
Mwaka 1971 ulikuwa mwaka wa nne tangu sheria ya utoaji mimba itungwe nchini Uingereza na hivyo vilikuwapo vituo vingi vya kutolea mimba. Mchumba wangu alinipeleka kwenye kituo kimojawapo cha kutolea mimba. Nikiwa nimejawa na tahayari, huzuni, upweke na woga wakati huo, nilijiuliza maswali mengi kuhusu mchumba wangu. Nikiwaogopa wazazi wangu ambao wangesikitika kama ningewaeleza mawazo hayo ya mchumba wangu, niliamua kwenda mbali ili kutunza siri na kujificha kutoka ukweli niliotaka kuufanya. Ili kukubali wazo hilo la mchumba wangu niliacha kuita mimba hiyo mtoto, badala yake niliita ni mkusanyiko wa seli tu. Katika chumba cha kutolea mimba washauri wa utoaji mimba walinihakikishia kuondoa hofu kwani katika umri wa majuma 11 tu hiyo haikuwa mimba bali damudamu tu. Ili kufanikisha ukatili wa kumwua mtoto kabla ya kuzaliwa lazima kwanza mtoto huyo adunishwe (dehumanized) ili aonekane kama siyo binadamu (dehumanization). Baada ya mimba kutolewa daktari (yule mwuaji) alisema kila kitu kilikuwa tayari na kwamba nitarajie kupata watoto wengi baadaye. Nilikuwa nafikisha miaka 21 wakati natoa mimba na sikuweza kufurahia sherehe iliyoandaliwa kwa ajili yangu, hisia kali za kujikatalia zilianiandama.
Wakati narudi nyumbani na mchumba wangu, hatukuongea chochote kuhusu tendo nililofanya. Niliendelea naye kimapenzi kwa siku nyingi zilizofuatia. Kwa kuficha aibu niliamua kuolewa naye; lakini kabla ya ndoa iligundulika nilikuwa na uambukizo katika mrija wa uzazi (salpingitis) ambao ulikuwa ni matokeo ya utoaji mimba. Maumivu ya ugonjwa huu yalikuwa makubwa na nilitibiwa kwa dawa kali (anti-biotics) za kuondoa ugonjwa huo. Miezi michache baada ya ndoa yetu, nilipata uja-uzito tena, lakini mimba ilikuwa inakua ndani ya mrija wa uzazi (ectopic pregnancy). Nikiwa hospitalini kwa matibabu walinifanyia operesheni ya kuondoa mimba hiyo na kuondoa mrija wa tumbo la uzazi. Baadaye walinieleza kuwa kwa kuwa mrija wa uzazi uliobaki ulikuwa umeharibiwa sana na ugonjwa niliopata, basi nisingeweza kupata mimba tena. Hata hivyo kwa vile nilikuwa na umri mdogo wa miaka 23 tu hawakuondoa ule mrija wa uzazi. Wakati wa mahangaiko hayo mume wangu alikuwa na kimada wa pembeni na hatukuwa na muda wa kuzungumzia bahati yangu mbaya ya kuukosa umama. Ndoa yetu ilivunjia miezi 13 baada ya kufunga. Niliacha kazi kwani akili yangu ilikuwa haifanyi tena kazi vizuri – nilichanganyikiwa.
Kilichofuatia baada ya hapo ni kunywa na uasherati. Mawazo ya
kujiua na
kujichukia wenyewe na kila mtu yalikuwa yananitesa sana.
Baada ya kupata mume wa pili nilijiona nimesalimika. Kama mwujiza nilipata tena uja-uzito. Nilijiona kuwa Mungu ana mkono wake katika maisha yangu; nilijifungua mtoto wa kiume na mwenye afya nzuri, Benjamini ambaye alikuwa kama mboni ya jicho langu.
Badala ya furaha ya kuwa na mtoto, sikuwa na uhusiano naye wa karibu sana. Siyo kwamba sikumpenda, bali niliogopeshwa na hali ya
kujihisi kuwa mimi si mama wa kweli; nilikuwa
najihisi kama nataka kumdhuru au
kuvunja mwili wake mdogo au
kwamba nitampoteza.
Kutokana na hali hizo nililazimika kumpenda hata kama ningempoteza. Sasa nina mahusiano mazuri naye ingawa hali ya kujisikia mkosaji itokanayo na kushindwa kwangu kuhusiana naye kama mtoto wangu halisi haikwisha. Jambo la kushangaza ni kwamba sijawahi kujisikia mkosaji kwa mimba yangu iliyoharibika wala ile iliyouawa kwa vile ilikuwa inakua ndani ya mrija wa uzazi, bali ni lile tendo la utoaji mimba. Kilichonishangaza zaidi ni kuwa hata kabla sijamweleza kuhusu tendo langu la kutoa mimba, Benjamin alikuwa anaota ndoto za kuweweseka kuwa nilikuwa namfukuza nikiwa nimebeba kisu, nikitaka kumwua. Ndogo hizo ziliisha baada ya kumweleza kuhusu utoaji mimba niliofanya na kumhakikishia kuwa nilikuwa nampenda kweli kama mtoto wangu.
Wakati huo huo nilikuwa na
matatizo ya usingizi
kula
fikra kali na
kusikia vilio vya watoto wachanga
ndoto za vitoto vilivyopajipanga katika mistari vikiwa vimefungwa minyororo
Ndoa yangu ya pili ilivunjika baada ya miaka mitatu na halafu hali ya kweli ya
kujichukia ilinijia pamoja na
maelekeo ya kujinyonga
Baada ya kushindwa ndoa mbili nilijihusisha na kikundi cha kanisa kinachowasaidia wanawake waliotoa mimba kuondokana na huzuni itokanayo na kuvunjika mahusiano ya kimapenzi. Nilidhani kinajishughulisha tu na kifo, talaka, kutengana, lakini kadiri masomo yalivyoendelea nilizama ndani zaidi na kugundua kuwa kilichokuwa kinanitesa ni utoaji mimba. Katika kujikatalia nilizoea kuita kitendo hicho ‘katizo la mimba’ [termination of pregnancy] na siyo ‘utoaji mimba’ na sasa nilikuwa najikisia mateso hayo yalikuwa yanatoweka taratibu.
Nilipata ushauri kutoka kwa ndugu kuhusu madhara ya utoaji mimba, lakini sikuweza kuamini, kwani nilikuwa najihami kutokana na aibu. Kaka yangu Christopher alijihusisha na utume wa utetezi uhai na akanisihi niangalie filamu ya “Silent Scream” [Kilio Kisichosikika] (Filamu hii inamwonyesha Dokta Bernard Nathanson, ambaye alijenga kliniki ya kwanza kubwa ya kutolea mimba nchini Marekani na alipata kuua watoto elfu sitini katika kliniki hiyo. Siku moja alipoangalia kipimo cha ‘utra sound’ wakati akimpima mama mja-mzito na kuona jinsi mtoto anavyojimudu tumbonni, na alipoangalia picha ya mtoto anayeuawa tumboni, aliacha kazi hiyo, akabatizwa na akatengeneza filamu hiyo ya ‘Silent Scream’ ambamo anaeleza hatua kwa hatua jinsi mtoto anavyouawa kwa kutumia vifaa mbalimbali. Dokta Bernard Nathanson alifariki dunia miaka miwili iliyopita, lakini filamu yake bado inaendelea kuwa zana nzuri ya kufundishia thamani ya uhai wa binadamu na unyama wa utoaji mimba)
Ilikuwa ndiyo filamu pekee niliyowahi kuiona, ingawa nilifumba macho kwani ilikuwa inaniumiza sana. Niliporudi nyumbani niliandika shairi nikieleza, kwa mara ya kwanza, mambo niliyotenda. Nilipoeleza kwamba niliangalia filamu ya “Silent Scream” wakati wa ushauri nasaha, mshauri nasaha aliniuliza;
“Ulijisikiaje”?
Nilimjibu kwa hasira, “Unadhani nilijisikiaje? Nilimwua mtoto wangu”.
Ingawaje nilijua sikumwua kwa mkono wangu, lakini nilijihisi kuwa ni mimi ndiye niliyeua. Baada ya kulia sana, nilizika habari hiyo akilini mwangu kwani sikuweza kuishinda tendo hali halisi ya huzuni iliyonikabili.
Mwaka 1985 nilihudhuria kwa mara ya kwanza kongamano la utetezi uhai lililoandandaliwa na SOCIETY FOR THE PROCTECTION OF UNBORN CHILDREN (SPUC) na huko nilikutana na Olivia Gans, mwanzilishi wa shirika la “American Victims of Abortion”. Wakati anashuhudia maisha yake na kuibua unyama wa utoaji mimba nchini Marekani, nilifikiri anaongea juu ya maisha yangu. Nilitaka kulia na kupiga mayowe, lakini nikasema mimi si mwenda wazimu. Nilikuwa na maumivu makali yasiyoweza kuelezeka. Nami nikajitokeza kuongea kuhusu masaibu yangu na nilitaka watu nchini kwangu Uingereza wafahamu kinachoendelea ndani ya vyumba vya kutolea mimba. Niligundua kuwa sikuwa peke yangu, na baada ya kuandika makala katika jarida la Bella, nilipokea simu simu nyingi kutoka kwa wanawake waliokuwa na matatizo kama yangu. Nikaelewa kuwa uponyaji unatokana na kuwa pamoja na wanawake wegine wanaoteseka na kuvunja hali ya kujitenga na kuyapa jina mateso yanasokusibu.
Katika kufuata hatua za ushauri nasaha na uponyaji nilitambua dhambi yangu ya ‘kuua mtoto wangu’ – utoaji mimba, hatua kwa hatua nilifaulu kumpatia jina mtoto wangu niliyemwua (ambaye naamini alikuwa msichana), nilimruhusu aende na nikamwaga. Zaidi ya hayo katika maumivu yangu nilipata nafasi ya kumlilia mwanangu Anna ambaye nilimwua katika tendo lile la utoaji mimba. Nilikuwa namfikiria Anna alipotimiza miaka 21 ya kuzaliwa kwake, siku ambayo niliitumia kwa kumshukuru Mungu kwamba Anna alikuwa sehemu ya maisha yangu. Na kwa kweli nilijisikia furaha kwa sababu niliamini kuwa Anna amenisamehe.
Mtu aliyekuwa mgumu kusamehe alikuwa ni mimi mwenyewe. Ilinipasa nijisamehe mimi mwenyewe na nikapata nafasi ya kumsamehe kila mmoja aliyehusika katika tukio la kumwua Anna: madaktari wote, manesi wote, shirika la “Britishi Parenthood Association”. Nilitaka wote waonje mateso yangu, waelewe kuwa alikuwa mtoto wangu. Ukidumu katika machungu yaliyokupata utajiumiza mwenyewe.
Imenichukua miaka 21 kupona madonda ya utoaji mimba, lakini kwa kufanya hivyo nimeonja msamaha na upendo ambao hakuna binadamu mwingine angeweza kunipatia. Katika uchungu wa upweke, mara nyingi nilikuwa nalia, “Hivi watu wanatambua kweli kwamba kitu hiki kidogo kilikuwa mtoto hai – mtoto wangu?” Katika maumivu yale nilimlilia Mungu: “Unajua kuwa huyu alikuwa mtoto wangu?”
Mara nilimsikia Mungu akijibu moyoni mwangu: “Ndiyo, Bernadetta, najua. Na nakusamehe mara moja”
Baada ya mahangaiko ya muda mrefu Bernadetta alipata uponyaji, na alipata tafsiri tofauti ya watu aliowafahamu na hata vitu alivyovijua. Baadaye alikuwa mshauri nasaha na mponyaji akawasaidia wanawake wengi walioteseka kama yeye. Na anasimulia kuwa katika wanawake wengi aliowafanyia ushauri nasaha kiasi cha asilia 90 yao walitoa mimba kwa ajili ya kumridhisha mtu fulani – mume, mshikaji, wazazi au makundi rika.
Shairi ambalo Bernadetta aliliandika linaitwa, “I cannot put flowers on your grave”, (Siwezi kuweka maua katika kaburi lako).
LAANA YA UTOAJI MIMBA
KWA WAMTOTO WALIONUSURIKA
Tuanze mada yetu kwa kurejea kisa cha Bernadetta Thompson wa Uingereza, yule ambaye baada ya kuharibika mimba yake ya kwanza, na kumwua mtoto wake wa kwanza [ambaye sasa angekuwa wa pili] alikabiliwa na laana mbalimbali, zikiwamo za kushindwa kumshika mtoto mchanga, kuwa na maelekeo ya kujiua, kujichukia mwenyewe na kila mtu, kujihisi kuukosa umama wa kweli, kujihisi kutaka kumdhuru mtu mwingine, kujihisi kupotelewa na kitu fulani, kujihisi mkosaji, fikra kali, kusikia vilio vya watoto wachanga na ndoto za vitoto vilivyojipanga katika mistari vikiwa vimefungwa minyororo. Baada ya mikasa hiyo miwili, Bernadetta alibahatika kujifungua mtoto na kumwita jina lake Benjamin. Akiwa bado mtoto na katika hatua zake za kukua Benjamin alikwa anaota ndoto za kuweweseka kuwa alikuwa anafukuzwa na mama yake aliyekuwa ameshika kisu akitaka kumwua. Ndoto hizi za Benjamin ziliisha pale mama yake alipomfahamisha alikuwa ametoa mimba, yaani alimwua kaka yake. Kisa hiki kinatueleza kuwa damu ya mtoto anayeuawa katika tendo la utoaji mimba inalia katika nafsi za watoto walio hai ambao wamezaliwa na mama huyo.
Inafaa sasa tueleze maana ya watoto walionusurika. Je, ni akina nani hawa? Je, wewe waweza kuwa mmoja wapo?
Watoto walionusurika ni:
wale waliozaliwa baada ya kushindikana jaribio la kuwaua [kimwili]
wale waliozaliwa baada ya wazazi wao kutishia kuwaua [kwa maneno]
wale waliozaliwa kabla au baada ya mwenzao wa mama mmoja kuuawa
wale waliozaliwa katika mazingira ambapo wenzao wengi wanauawa
wale wanaozaliwa katika nchi ambayo imepitisha sheria ya kutoa mimba
Katika dhati yake kabisa, watoto hawa hawajafanya kosa linalostahili adhabu, bali laana hii inamhusu mama aliyeua watoto wake kwa njia ya utoaji mimba. Katika mazingira haya, laana hii ya utoaji mimba inakuwa na matokeo mabaya kwa watoto wanaozaliwa na mama huyu mwuaji, ni kama vile mama huyu anarithisha laana yake. Kwa hiyo mtoto anaambukizwa laana ya mama yake na inajitokeza kwa namna mbalimbali.
Kwa pande mmoja watoto walionusurika hawaoni thamani ya kuishi, hawaoni thamani ya uhai wao au wa wengine. Mara kadhaa na katika mazingira tusiyoweza kutegemea unaweza kumsikia mtoto au hata mtu mzima akimwambia mwezake, NITAKUUA. Unajiuliza ‘kauli hii ina maana gani’, au pengine unaweza kujiuliza, ‘je kuna kitu gani kilichosababisha hasira ya kiwango hiki cha mtu kutamka au kutishia kumwua mwingine?’ Na siku hizi tunashuhudia vitendo hivi katika matukio ya yutanasia, ambapo mtu, kutokana ama na ugonjwa au umri kuwa mkubwa anamwomba daktari au mtu mwingine amwue ili kuondoa mateso; au pengine daktari baada ya kumhudumia mgonjwa kwa muda mrefu pasipo matumaini ya kumponyesha anaweza kushauri mgonjwa wake aombe kifo kama tiba kwa ugonjwa wake.
Kwa upande mwingine, watoto hao wana hofu ya kufa na hivyo wanashindwa kufanya mipango ya maisha ya baadaye wakifikiri kuwa wanaweza kuuawa wakati wowote. Tukumbuke kisa cha Benjamin aliyekuwa anaota anakimbizwa na mama yake aliyetaka kumwua. Katika hali ya namna hiyo inakuwa vigumu mtu kuweka mipango ya maisha kwa vile hofu ya kifo hutawala maisha yake. Na katika misiba watu wa aina hiyo wanaweza kulia sana. Ziko sababu nyingi za watu kulia sana katika msiba, pengine marehemu alikuwa tegemeo katika familia, au mume/mke, ndugu, jirani au rafiki. Lakini kwa mtu aliyenusurika kifo kutokana na utoaji mimba uliofanywa na mama yake, kilio chake kinaweza kuwa kinatokana na sababu kwamba, yeye anajiweka kama ndiye aliyekufa. Hii ndiyo hofu ya kifo.
Wanashindwa kuwaamini na kuwathamini wazazi wao. Kwa kawaida, watoto huwaheshimu na kuwathamini wazazi wao kutokana na silika ya kimahusiano kidamu, imani na mila zetu. Katika amri ya nne Mungu anawaamuru watoto kuwapenda na kuwaheshimu baba na mamaili wapate kuishi miaka mingi na heri duniani. Kwa hiyo upendo na heshima kwa wazazi unapata matunda yake katika tuzo. Hatutegemei kuwaona au kuwasikia watoto wakiwadharau au kuwatukana wazazi wao. Lakini vitendo vya utoaji mimba vimezua laana kwa watoto ambao sasa huwatukana, kutishia kuwaua (au hata kuwaua), kuwatelekeza na hata kuwapiga wazazi wao. Moyo wa ukatili wa mama umehamia kwa mtoto ambaye nayo anaudhihirisha kwa kumgeukia huyo mama mwovu. Katika matendo kama hayo mara nyingi jamii imeelekeza lawama kwa watoto ambao wanapachikwa tuhuma mbalimbali. Lakini leo nataka tutafakari upya tuhuma hizo. Mtoto aliyenusurika hawezi kumthamini mama yake kwani anajihisi kuwa mama yake ni mkatili na mwuaji, hata kama hajaambiwa kuwa kaka zake au dada zake waliuawa. Kwa hiyo unaweza kushuhudia mtoto akimshikia kisu/shoka/upanga mama yake kutaka kumwua au kumwua kabisa. Na sisi tunashangaa inakuwaje? Jibu limo katika laana ya utoaji mimba. Jambo hilo lilifanyika kwa siri lakini matokeo yake yanakuwa ya wazi.
Wanakuwa wanyonge na wenye hasira kali. Katika uumbaji Mungu alimwumba kila binadamu akiwa mwenye furaha, amani, upendo na tunu nyinginezo. Lakini katika hali ya utoaji mimba, mama anafuta hizo tunu njema za Mungu na kupandikiza kwa watoto wanaozaliwa kabla au baada ya mwenzao kuuawa tunu hasi za unyonge na hasira kali. Unyonge unatokana na sababu kwamba mwenzake ameuawa. Huu ni unyonge wa kila mfiwa. Hasira kwa sababu kifo hicho kimesababishwa na ukatili wa mama. Kwa hiyo uzao unajenga hasira sio kwa mama huyo tu, bali kwa kila mwanamke. Hata watu wasiohusika watamwona mtoto huyo kuwa mwenye hasira zinazoelekezwa kwa kila mmoja. Wakichokozwa kidogo tu, basi ngumi zinaanza hapo hapo au majibishano ya matusi. Darasani watoto wa aina hiyo wanakaa nyuma kwenye kona. Wakiwa nje wanajitenga na wengine, hawataki shirika. Walimu wakiwatambua watoto wa aina hiyo wafanye jitihada za kuwasaidia badala ya kuwaadhibu au kuwaacha. Uhusiano wa mwalimu na watoto hao unaathiri sana maendeleo yao kielimu.
Wataalamu wengine wameonyesha laana zifuatazo zionekanazo kwa mtoto aliyenusurika:
Anakuwa na chuki kwa mama; hana upendo kwake; mama yake anaweza kujihisi vibaya
Hamwamini mama, anajitenga na kukimbilia kwa baba yake [kama yupo]. Muda mwingi anakuwa karibu na baba yake kuliko mama yake
Anajenga chuki kwa jinsi ya kike na kutowathamini wanawake
Wanaweza kuwaasi wazazi wao na kujishikiza katika makundi ya watoto waasi wenzao [k.m. watoto wa mitaani]. Wakiwa nyumbani watoto hawa wanajihisi kukataliwa, wanajisikia huzuni, wanakuwa na hasira. Suluhisho pekee ni kutoka nyumbani na kwenda kuishi mbali na wazazi ambao wanawaona kuwa ni wauaji. Katika kufanya hivyo, huko waendako wanakutana na watoto wenzao waliotoka nyumbani kwao kutokana na sababu hizohizo au nyingine, basi wanaungana na kujenga urafiki. Katika hali ya kukosha utambulisho wa wazazi wao watoto hawa sasa wanakabiliwa na maisha mapya yasiyokuwa na makazi wala wazazi.
Katika hali hiyo, tunahitaji washauri nasaha kuweza kuwasaidia watoto hao kuwarudishia ubinadamu waliopoteza; tunahitaji mashirika ya hiari yanayoweza kuwahudumia watoto hao katika upendo na kuwarejeshea malezi yaliyopotea kutoka kwa wazazi wao; tunahitaji serikali kuwa na mikakati ya muda mfupi na muda mrefu ya kuwasaidia watoto hao. Lililo kubwa kwa upande wa serikali ni kudhibiti vitendo vya utoaji mimba.
Wana maelekeo ya kujiingiza katika vitendo vya ushoga na matumizi ya pombe na dawa za kulevya. Vitendo vya ushoga vinatokana na kunyanyaswa na kutelekezwa utotoni. Watoto walionusurika hawajisikii vema kubaki na wazazi wao kwa vile wanajisikia vibaya wakihisi ukatili uliopea wa wazazi wao. Kwa hiyo, watoto hawa wanajitambulisha kimapenzi wa wenzi wa jinsi moja ili kufidia umama au ubaba uliopotea. Pombe na madawa ya kulevya huwaletea faraja potofu na hatimaye wanazidi kuzama katika lindi la uhayawani.
LAANA YA UTOAJI MIMBA
KWA BABA WA MTOTO
Wengi wanafikiri kuwa laana ya utoaji mimba inamkumba mama mzazi wa mtoto aliyeuawa tu kwa vile yeye ndiye anabeba mimba ile, na ni yeye ndiye afanyaye uamuzi wa mwisho wa kumwua mtoto wake. Wengi walimsahau baba wa mtoto. Ni siku za hivi karibuni tu uchunguzi na tafakari zimeanza kugundua kuwa hata baba ambaye mtoto wake ameuawa kwa njia ya kutoa mimba anakumbwa na laana. Mawazo ya awali yaliyomwondoa baba wa mtoto kutokana la laana ni kuwa, yeye hakuwa sehemu ya utoaji mimba. Ni kama vile alikuwa mbali na janga hilo. Lakini polepole wanazuoni wa masuala ya saikolojia ya wanaume ambao watoto wao waliuawa kwa njia ya utoaji mimba wametupa mwanga kuwa, mbali na kuwaondoa wanaume katika laana, wanaume nao wanakumbwa na laana hiyo. Tuchukue mfano mdogo tu katika maisha ya kawaida; tuseme mtoto amefariki katika familia. Je wafiwa wa mtoto huyo, yaani baba yake na mama yake wanajisikiaje? Jibu ni kuwa kila mmoja wao anaathirika kwa namna fulani, na mara nyingi, namna hizo zinafanana; kwa mfano, uchungu, kumbukumbu, ndoto za maono, kujihisi kupoteza kitu fulani maishani na kuonja dhahiri pengo kati ya uzao na uzao. Ni kwa misingi hiyo, ndipo sasa tunajadili laana inayomkabili baba wa mtoto aliyeuawa kwa kutolewa mimba.
Kujisikia kukosa heshima ya ubaba na kuitwa baba fulani. Kila baba mzazi anaona fahari juu ya uzao wake. Ni sifa kubwa kwa mwanaume aliyefikia utu-uzima na/au ameoa kuitwa baba wa mtoto fulani. Heshima hii kwake humaanisha jambo moja kubwa, mwendelezo wa jina la ukoo wake ambalo litadumu kizazi hadi kizazi. Kwa upande mwingine, baba mzazi anajisikia vizuri na kuonja faraja iwapo mtoto aliyemzaa anapata nafasi nzuri katika maisha yake, yaani, kuajiriwa, kuwa mwanasiasa mashuhuri, kuwa mhudumu wa kanisa kama mtawa, padre, mchungaji, askofu na hata kuwa mkulima hodari, mvuvi hodari au mfugaji hodari. Mtoto anasikia fahari kuitwa mtoto wa baba fulani na wa ukoo fulani. Inapotokea mtoto anauawa kabla hajazaliwa, mategemeo haya ya baba hupotea na ndipo baba anajisikia kukosa heshima ya kuitwa baba fulani.
Kujisikia mtu mwenye huzuni, aibu, mkosaji, kukosa amani na mtu asiyefaa. Mtu anayepatwa na msiba hujisikia huzuni kutokana na kuondokewa na mpendwa wake. Hali kadhali katika hali ya kutoa mimba, baba wa mtoto anakuwa amepotelewa na mtoto wake, yaani ni mfiwa. Katika maisha ya kawaida, mfiwa hupewa pole na ndugu, majirani na marafiki. Lakini katika utoaji mimba, mfiwa, baba ya mtoto, hapewi pole, anakuwa amepoteza heshima. Aibu anayoipata baba inatokana na ukweli kuwa, jambo baya limetokea katika nafsi yake, yaani yametokea mauaji ya mtoto wake na heshima aliyoitegemea ya kuitwa baba inapotea na anajisikia kama vile amekuwa mshirika katika mauaji ya mtoto. Kama baba ameshiriki moja kwa moja katika ushauri, kutoa fedha za kumlipa mwuaji basi baba huyo atajisikia mkosaji na ndiyo maana anakosa amani na kuonekana asiyefaa mbele ya baba wengine. Na ndiyo maana, tusishangae, baba huyo anaweza kukabiliwa na ndoto za kuwewezeka. Wengine wanaweka kumbukumbu ya umri wa mtoto, tarehe mtoto alipouawa, na hata jinsi ya mtoto, yaani kama alikuwa mwanaume au mwanamke.
Hasira inayoelekezwa kwa wengine au kwake mwenyewe, na hata kukata tamaa. Hali hii inatokana na kujutia baada ya tendo la mauaji ya mtoto. Anaonja ubaya wa kumwua mtoto wake mwenyewe, hasa kama alishawishiwa na marafiki. Anazijutia fedha alizotoa kumlipa mwuaji. Hasira hiyo itaelekezwa kwa wale waliomshauri. Na kama alifanya uamuzi huo mwenyewe bila kushawishiwa, basi, yanapotokea mazingira ya kumbukumbu basi hali hiyo itaelekezwa kwake mwenyewe. Baba huyu anajihisi hafai tena kuitwa baba na asiyekuwa na faida kama baba wa kweli. Hata kama baadaye atapata watoto wengine, bado atajisikia hasira kwa kuwa mtoto wake mmoja aliuawa kwa njia za kikatili.
Ni hali hiyo ndiyo inamfanya ajitenge na watu, hasa marafiki na ndugu wanaofahamu jambo hilo, na hata kama hawafahamu, baba huyo atajihisi tu kuwa labda watu wanafahamu. Kicheko cha majirani kinaweza kumsumbua sana akidhani wanamcheka yeye. Daima anakuwa ni mtu wa wasiwasi asiyemwamini mwingine kwa vile anadhani wanafahamu tukio hilo la mauaji ya mtoto wake.
Kukimbilia kwenye pombe na dawa za kulevya kunatokana na baba huyo kukata tamaa, kufikiri watu wanafahamu na wanamcheka na hali ya kujisikia kuwa amekuwa mkatili wa kupindukia, hata kumwua mtoto mchanga asiyekuwa na hatia wala uwezo wa kujitetea. Huivuruga akili yake kwa pombe na dawa za kulevya akiamini kuwa vinamsaidia kusahau machungu yanayomsibu. Ulevi wa muda unamfanya apate marafiki bandia wanaomfariji, naye anajisikia vizuri na kudhani kuwa matatizo yake yamepatiwa ufumbuzi. Pombe au dawa za kulevya vinapoisha nguvu, akili yake hurudi katika hali ya kawaida na maisha yake yanarudia hali yake ileile. Basi ni mzunguko wa laana juu ya laana; laana ya kushiriki katika mauaji mtoto na laana ya ulevi.
Uchungu huu unaompata baada ya kutambua kuwa mtoto wake ameuawa, na hasa kama mama wa mtoto alifanya hivyo bila kumshirikisha, unamfanya baba huyu kuharibu mahusiano yake na wanawake anaokutana nao. Haoni tena thamani ya umama katika mwanamke. Anaweza kuhisi kuwa kila mwanamke ni mwuaji. Na hali hii ikiendelea, mwanaume huyu anaweza kushindwa kuoa, kwa hofu kuwa ‘huyu naye atamwua mtoto wangu’. Baba wa mtoto aliyeuawa anaweza kujenga hali ya kutomwamini mama watoto wake.
Ndiyo maana wanaume wa aina hiyo wanakuwa na maelekeo ya tabia na vitendo vya kishoga kwa kuogopa kumpa mimba mwanamke. Daima wanafikiri kuwa tendo la ndoa likitendeka litaleta uzao wa binadamu mpya katika tumbo la mama na mama huyo atamwua huyo mtoto. Basi wanaona kuwa suluhisho lake ni kutojihusisha na wanawake kimapenzi na badala yake kuamua kuhusiana na wanaume wenzake kimapenzi. Hali hiyo inazua laana nyingine, yaani, kufanya tendo la ndoa kwa njia ya haja kubwa. Tusishangae tunaposhuhudia kushamiri kwa wimbi la ushoga duniani na ndoa za watu wa jinsi moja. Watu wanafikiri kuwa vitendo vya ngono kwa njia ya haja kubwa vina hadhi ileile ya vitendo hivyo kwa njia ya kawaida. Vitendo hivi vimekuwa ni vya kawaida hata katika ndoa ambapo wanandoa wanatumia kama njia ya uzazi wa mpango. Wengine wanafikiri kuwa vitendo vya ngono kwa njia ya haja kubwa vinaleta msisimko zaidi, wakisahau ukweli kuwa ndiyo njia kubwa ya kueneza magonjwa ya zinaa.
Tabia hii sasa imetapakaa duniani kote, na kwa njia ya mitandao ya intaneti watu wanajifunza na hivyo kudhani kuwa ni fasheni mpya ya mahusiano. Tafiti mbalimbali zinaonyesha kuwa magonjwa ya zinaa yameongezeka kwa kiasi kikubwa na kwa kiwango kikubwa kutokana na ukengeukaji huu wa tendo la ndoa. Huko Marekani, kabla ya kushamiri kwa vitendo hivi kuanzia miaka ya 1960 zilikuwapo aina tano tu za magonjwa ya zinaa. Lakini baada ya kushamiri vitendo hivi idadi ya magonjwa ya zinaa imeongezeka kufikia zaidi ya 50. Ndiyo kusema kwa kadiri watu wanavyokengeuka katika mpango wa Mungu wa tendo la ndoa, ndivyo hivyo wanavyojichumia laana mbalimbali.
Kwa kawaida mfiwa hubaki na kumbukumbu ya muda mrefu ya yule mpendwa wake aliyekufa. Ingawaje maono na kushituka yanaweza kutokea kwa yeyote aliyefiwa, lakini yanakuwa makali zaidi kwa mtu aliyeua kwa kukusudia tena kwa mtu ambaye hakuwa na hatia. Na hali hiyo ndiyo inamfanya kupoteza usingizi [wengine wanasema ‘analala macho’]. Mahangaiko ya mtu aliyeua yanakuwa makubwa. Tunashuhudia katika tukio la mtu kumwua mwingine, hata kama atakimbia na kuishi mbali na tukio, dhamiri yake itamsuta daima hadi anakamatwa. Dhambi ya mauaji ni kubwa na kama nilivyosema huko nyuma katika mada hii, ni dhambi inayodai kisasi.
LAANA YA UTOAJI MIMBA
KWA ALIYEUA [DAKTARI/MGANGA AU MWINGINE YEYOTE]
Siku hizi katika mafunzo ya uganga/utabibu, utoaji mimba ni moja ya masomo yanayofundishwa na mtahiniwa hapatiwi cheti kama hajafaulu somo hilo. Somo hilo, licha ya kufundishwa kinadharia, linawataka wanafunzi kulifanya pia kivitendo. Kwa hiyo mwanafunzi anapohitimu tayari anakuwa amejengewa mazingira ya kuona kuwa mauaji ya watoto kabla ya kuzaliwa ni jambo la kawaida. Na tena vitendo hivyo vinajengewa mazingira ya kutendeka hata kama katika misingi ya kimaadili yangeonekana kupingana na silika ya binadamu ya kupokea, kupenda na kulinda uhai. Hoja zinajengwa ili kuhalalisha mauaji hayo – mimba inadhohofisha afya ya mama; mimba inahatarisha uhai wa mama; mimba imetokana na ubakaji; mimba ni ya ndugu; ni afya ya kizazi; ni haki za vijana. Vitendo vya mauaji ya watoto vinapofanywa kuwa sehemu ya mafunzo ya udaktari/utabibu na yaposhamiri katika jamii na kuwa sehemu ya utamaduni wa maisha ya watu, wauaji hujenga tabia ya ukatili na kukosa huruma; hawawezi kusikia sauti ya kilio cha mtoto. Wauaji hao wanaona kuwa kutoa mimba ni biashara nzuri inayowapatia malipo makubwa na ndiyo maana wanaitetea kwa nguvu zao zote. Badala ya kuwaona matabibu wetu kuwa watu wa kurejesha afya iliyodhohofika kwa magonjwa mbalimbali, sasa wanaonekana wauaji, siyo tu watoto ambao bado hawajazaliwa, bali pia wa wagonjwa wanaohitaji huduma yao, walemavu na vikongwe. Hawathamini tena uhai, ambao sisi watetezi wa uhai tunaujali kama ni zawadi ya Mungu kwa binadamu na ni mali yake Mungu, kwani ndiye aliyeuumba na ndiye mwenye mamlaka ya kuuondoa.
Na wakifikia hali ya kutothamini tena uhai wa binadamu, wauaji wanakuwa wamelewa mauaji; ndiyo maana baada ya kuua mtoto mmoja wataua na wa pili, wa tatu, wa nne – hatimaye yanakuwa mazoea. Watu wanaojihusisha na mauaji ya watoto kabla ya kuzaliwa wanakuwa na lugha na tabia moja duniani kote na kwa ujumla wao wanaunda kundi moja la wauaji na watetezi wa kifo. Hao ndio wanaunda utamaduni wa kifo. Ndiyo maana, nadhani, siku hizi kuna kushamiri kwa tiba kwa dawa za asili; na pengine ndiyo maana wimbi kubwa la watu linakimbilia kwa Yesu kwa ajili ya kupata uponyaji, siyo tu wa mwili, bali pia wa roho. Kushamiri kwa mapepo kunatokana na kumpatia nafasi Ibilisi katika maisha yetu kwa njia ya mauaji, hasa ya watoto ambao bado hawajazaliwa. Na ndiyo maana Ibilisi naye hachezi mbali. Yu karibu nao, akiwachochea kuua zaidi, kwani damu ya watoto wachanga ndiyo malisho yake mazuri.
Madaktari watoaji mimba na watoaji mimba wengine wote, wanakuwa wakali, hali inayotokea kama njia ya kujitetea dhidi ya wale wanaowapinga. Mara nyingi wapinzani wa utoaji mimba, yaani watetezi uhai, kama wewe na mimi, wanaishia kushtakiwa mahakani kwa kuonekana wanaingilia uhuru wa mtu binafsi wa kufanya maamuzi yake. Katika nchi yoyote ambayo imehalalisha utoaji mimba, linakuwa ni kosa la jinai kupinga vitendo vya utoaji mimba. Sheria inawalinda wauaji na kuwaadhibu wale watetezi uhai, ambao kwa mujibu wa sheria wanaonekana wamevunja sheria. Kule Afrika ya Kusini, sheria ya utoaji mimba ni kali kiasi kwamba inaweza kumfunga jela miaka hadi 10 daktari anayekataa kutoa mimba. Kule China, mwanamke anayebeba mimba ya pili au zaidi anakabiliwa na kifungo, mateso na hata kifo. Wanandoa kule China wanapaswa kuomba kibali kutoka serikalini cha kuzaa mtoto wa pili. Sheria za China zinataka kila familia kuzaa mtoto mmoja tu, na upendeleo umewekwa kwa uzao wa watoto wa kiume. Kwa sasa hivi Wachina wanaume zaidi ya milioni 30 wanakosa wanawake wa kuwaoa kwa sababu hakuna wanawake wa kuwaoa, hali inayotokana na upendeleo wa utoaji mimba za watoto wa kike.
Madaktari wanaojihusisha na vitendo vya utoaji mimba wanafanya biashara zao kwa siri, hawapendi kujulikana na wengine. Wanajenga tabia za woga na aibu kwani dhamiri zao zinawasuta. Hawapendi wajulikane kama ni wauaji. Watu hao hushinda katika vilabu vya pombe na baa, wakivuta sigara na kucheza ‘pool’. Ni waongeaji na wachekeshaji sana baada ya akili yao kuvurugwa na pombe. Hayo yanafanyika kama kinga dhidi ya aibu, na ni njia yao ya kujificha. Kujiingiza katika ulevi kunafanyika kama tiba ya maumivu wayapatayo kutokana na ukatili wao. Nilipokuwa mdogo nilikuwa nasikia watu wakisema, daktari fulani anafanya upasuaji mzuri kama amelewa. Kwa hiyo ulevi ulichukuliwa kama dawa ya daktari ili aweze kutibu vizuri. Leo ninapoyatafakari maneno yale ya utotoni, naanza kujiuliza, kweli ulevi unamwezesha mtu kufanya kazi yake vizuri? Pengine jambo lile lililofichika, sasa linafichuliwa, kwamba daktari huyo alikuwa mtoaji mimba. Yawezekana damu ya mtu aliyekuwa anamfanyia upasuaji ilikuwa inamfichulia kumbukumbu ya watoto wachanga aliokuwa anawaua. Lakini, tuseme labda, ulevi ulikuwa unamwezesha kuondoa huruma ya kumdhuru mtu mwingine, kwani tiba ya upasuaji inahusisha kudhuru na umwagaji damu wa mtu mwingine. Kwa vyovyote vile ulevi unaleta usahaulifu wa muda na kwa wengine huwa kama tiba kwa jambo baya wanalofanya.
Kama ilivyo kwa mama, mtoto na baba, daktari naye anakabiliwa na maono, kuweweseka na kumbukumbu ya vitendo vyake. Ni silika ya kibinadamu inayorejesha mwangwi wa tendo baya lililotendwa. Hakuna awezaye kuepuka. Kama nilivyosema hapo awali, mwuaji hawezi kujificha. Hata kama atajificha kutokana na macho ya binadamu, hawezi kujificha machoni pa Mungu. Daima dhamiri itamwambia, ‘umeua…umeua…umeua’. Na ni hali hiyo ndiyo itamfanya aweweseke usingizini na kuweka kumbukumbu ya mauaji aliyofanya.
Watu hao hatimaye, wanaishi katika mgongano wa dhamiri kati ya wema na ubaya; uhai na mauti. Na katika hali hiyo hukwepa nyumba za ibada kwa vile wanaogopa kuumbuliwa imani zao. Pengine msongo wa mawazo ndio unawafanya wakimbilie kwenye pombe na sigara.
Kama ilivyo kwa mama, mtoto na baba, wauaji [madaktari au wengine] nao wanahitaji ushauri nasaha na uponyaji. Tunapenda kuwaalika kwetu, tutawasaidia. Mungu mwenye huruma na upendo hatawatupa kamwe. Maandiko Matakatifu yanatuambia kuwa Mungu humkaribisha kwake kila binadamu atubuye. Ili waonje huruma na upendo huu wa Mungu wanahitaji toba ya kweli. Hitaji la kwanza ni wao kutafakari moyoni mwao kwa lengo la kutambua makosa [dhambi] zao; hitaji la pili ni kudhamiria kuacha hayo makosa; hitaji la tatu ni kuamua kuondoka, yaani kuachana na hayo makosa; na hitaji la nne ni kutubu, yaani kuomba msamaha kwa Mungu na kwa wanadamu wote ambao wamewakosea; hitaji la tano ni kuwa kiumbe kipya katika ushirika na Mungu. Wauaji wote, wawe wahudumu katika fani ya utabibu; wahudumu wa dawa za asili au wengineo, wanatakiwa kuvunja laana inayowakabili – ukatili na mauaji ya watoto wasiokuwa na hatia. Kwa njia ya kupatiwa ushauri nasaha na uponyaji wa ndani na toba ya kweli, wanaweza kuvunja laana inayowabili. Wale waamini wakatoliki wakumbuke kuwa ukamilifu wa uponyaji unatolewa katika sakramenti ya upatanisho, ambapo kwa njia ya wateule wake, yaani makasisi, Mungu huondoa dhambi hiyo na kuvunja laana zote zinazomkabili mtu huyo. La msingi ni kuwa tayari kubadilika na ndipo Mungu hutoa bure baraka na neema zake.
LAANA YA UTOAJI MIMBA
KATIKA FAMILIA NA TAIFA
Tunapoangalia laana ya utoaji mimba hatuwezi kuacha kujadili laana inayozikabili familia na jamii kwa ujumla wake. Familia ndio taasisi ya msingi ambamo binadamu huzaliwa na kuwiwa nayo. Familia ndilo chimbuko la watu na taifa. Familia inapotindikiwa na wana-familia, ndivyo hivyo taifa linavyokosa watu. Familia inapokabiliwa na majeraha yanayojiegemeza katika ukatili wa kuua wanafamilia ambao hawajazaliwa, ndivyo hivyo moyo wa ukatili unavyodhihirika katika namii. Leo hii tunsihangae tunaposikia katika vyombo vya habari mama mzazi amemweka mtoto wake mchanga katika mfuko wa rambo na kumtupa vichochoroni au barabarani, au tunaposikia baba amemwadhibu mtoto wake kiasi cha kumjeruhi au tunaposikia mama amemchoma mtoto wake kwa moto kwa sababu ya kuiba shilingi mia tano au mtoto amezurura. Hii ndiyo laana inayozikabili familia nyingi leo. Tunatupiana lawama juu ya kuporomoka maadili yanayoathiri malezi ya watoto wetu, kama vile hatuelewi kwamba hali hiyo inatokana na laana ya kuua watoto wetu. Kama unaona watu katika taifa wameharibikwa kimaadili – mauaji, ufisadi, ukatili ulioelezeka, na matukio mengine ya ajabu, kama vile uporaji, umwagaji damu unaotokana na matumizi ya silaha za moto, ufahamu kuwa hali hiyo inaakisi laana kubwa iliyoikumba jamii hiyo.
KATIKA FAMILIA
Babu na bibi wanakata tamaa, hawaoni wajukuu wa kuwapokea na kucheza nao. Shangazi wanakosa wapwa, hakuna wa kutaniana naye. Katika Afrika faraja ya wazee ni kuona kizazi kinarithishwa kwa njia ya wajukuu. Uzao wa watoto ndio bima pekee na ya kuaminika katika maisha ya uzeeni. Katika hali ya utoaji mimba, siyo tu kwamba babu na bibi wanakosa wajukuu wa kucheza na kufurahi nao, lakini zaidi sana utoaji mimba unamaliza kizazi na ukoo. Hali hii ni kinyume kabisa cha shabaha ya uumbaji, ndoa na familia. Mungu, katika mpango wake wa uumbaji alitaka kizazi kiendelee kuwapo hadi kuijaza nchi kwa njia ya ndoa na familia. Wanafamilia wanapojihusisha na kusitisha uzao, si tu kwamba wanajimaliza wenyewe - wanajifuta katia sura ya dunia, bali zaidi sana wanakaidi amri ya Mungu Muumba.
Wimbi la utoaji mimba linaposhamiri, familia zinawaleta duniani watoto waliopondeka moyo, waliojeruhiwa kiakili. Na katika hali hiyo familia zinashuhudia kuzuka kwa vijana walio katili, wenye vurugu na hasira wakichokozwa. Huu ni ukatili wa wazazi unaopelekwa kwa watoto wao kwa sababu ya mauaji yanayofanyika katika familia. Watoto wanarithishwa tabia ya mauaji kutoka kizazi kimoja hadi kingine. Na katika hali ya kawaida kabisa tunashuhudia kuzuka kwa vitendo vya ukatili hata kwa makosa madogo madogo. Ukatili wa mama kwa mtoto, baba kwa mtoto, mume kwa mke, mke kwa mume, mtoto kwa wazazi wake. Mzunguko usiokwisha wa ukatili na mauaji. Na hatimaye, familia zinashuhudia kujengeka tabia ya kuwanyanyasa na kuwatelekeza watoto. Ndipo hapa tunapowapata watoto wanaoitwa wa ‘mitaani’ au wengine wanapenda kuwaita watoto hawa ‘wanaoishi katika mazingira magumu’
Utoaji mimba unapofanyika katika familia, laana yake hurithishwa kwa vizazi vinavyofuatia hadi vizazi vinne. Maana yake ni kwamba ukatili wa mama huyu mmoja utarithishwa kwa watoto wake, wajukuu wake, vilembwe wake na vilembekwezi wake. Hii ina maana kwamba tunapata mfululizo wa uzao wa kizazi cha binadamu walio siyo tu wakatili, bali pia kizazi kisichokuwa na huruma, kizazi cha mauaji, kizazi cha watu wasiokuwa na upendo katika maisha yao, kizazi cha watu ambao hawajali maisha yao wala ya wengine. Hiki ni kizazi cha hovyo kinachofurahia mauaji badala ya uhai. Ndiyo maana leo hii usishangae kuona familia chache ambazo hazijajihusisha kwa namna moja au nyingine katika suala la utoaji mimba. Katika familia nyingine imekuwa ni fasheni kuua watoto wao wasiozaliwa. Mama mzazi atamhimiza binti yake kuua mjukuu wake, eti ili binti yake ahitimu masomo yake. Usishangae mume akampatia mke wake fedha za kuua mtoto wao eti kwa sababu anaogopa aibu ya kuzaa katika mfupi mfupi. Na laana nyingine zinazojitokeza hazina maelezo ya wazi, kwa mfano mafarakano kati ya mume na mke au vurugu katika maisha ya wanafamilia. Na hapo inazaliwa hali ya kutoaminiana, kuogopana, kuhisiana vibaya – kwa ujumla wake kuvunjika siyo tu upendo wa kindoa, bali pia upendo wa kifamilia.
KATIKA MIUNDO YA JAMII
Nani atashangaa leo tunapoona watu wanafurahia matukio ya vifo; na hata kushabikia methali ya Kiswahili isemayo, ‘kufa kufaana’. Yawezekana methali hii ilikuwa inatumiwa katika maana nzuri na wahenga wetu, lakini katika kushamiri vitendo vya mauaji, watu wanashindwa kuwa na huruma katika matukio ya vifo na hivyo kifo cha mtu ni furaha kwa wanaobaki. Tunashuhudia pia leo hii watu wakizifurahia ajali kwa lengo la kupora mali ya majerushi au wafu. Matukio ya misiba haleti tena taswira ya uchungu na maombolezo, bali yamegeuka kuwa ya shehere, kula na kunywa, na hata kugawana mali ya marehemu kabla hata hajazikwa kunakofanywa na wana-ndugu. Katika matukio ya misiba zitaundwa kamati za mapambo, kamati za chakula, sare zitashonwa na watu watafika kwa wingi siyo kwa ajili ya kuomboleza, bali kwa ajili ya kusherehekea.
Katika kushamiri kwa vitendo vya utoaji mimba, watu hawana huruma tena na watu wenye ulemavu. Na hali hii imepelekea kuvunjika kwa miiko ya kale ya kuwalinda watu wasiojiweza/walemavu. Je, hatujashuhudia leo hii walemavu wa ngozi wakiwindwa na kuuawa? Je, hatujasikia watu na mashirika fulani yakiitaka serikali yetu kutunga sheria za kuwaua walemavu tangu wakingali matumboni mwa mama zao? Je, hatujashuhudia ukitolewa wito wa kuwaua watu wasiojiweza, kama vile wagonjwa mahututi na hata vikongwe. Dunia ya leo inashuhudia kuzuka na kushamiri kwa vitendo vya kuwaua watu ‘kwa kuwahurumia’ [yutanasia] na hata kuwaua watu wa dini au rangi nyingine.
Kilele cha kukosa tunu ya huruma katika jamii ni pale serikali inapotunga sheria za kutoa mimba. Serikali inapofikia kiwango hicho cha utendaji, kinawajengea watu wake moyo mgumu wakati wa mauaji ya watoto wachanga kiasi kwamba sasa linakuwa jambo lililokubalika kisheria. Mama Theresia wa Calcutta alipata kusema, ‘iwapo mama anaweza kumwua mwanaye wa tumboni, je, kitazuia nini sisi kwa sisi kuuana?’ Alisema kweli, tukiwa na tabia ya kuwaua watoto kabla ya kuzaliwa inakuwa rahisi kuana sisi kwa sisi kwa kisingizio chochote kile, kisingizio chaweza kuwa tofauti za kisiasa, tofauti za kiimani, tofauti za kiuchumi kati ya maskini na matajiri au hata tofauti za rangi. Kaini alimwinukia nduguye Abel kwa sababu tu ya kuona kuwa sadaka yake haikupata ridhaa mbele ya Mungu, wakati ile ya nduguye ilipata kibali. Ukazuka wivu, mauaji yakatokea. Herode aliua maelefu ya watoto kwa kwa sababu ya wivu akidhani miongoni mwa watoto hao yumo mmoja ambaye angechukua madaraka yake. Nasi tunawaua watoto kabla ya kuzaliwa kwa sababu ya wivu, chuki, uchoyo. Tunadhani wakizaliwa watapunguza pato letu katika maisha. Na tunapokuwa na moyo mgumu kwa watoto wachanga wasiozaliwa na ambao hawakukosea lolote, tutakuwa wagumu zaidi kwa wenzetu wanapotukosea.
Katika imani ya dini zote, utoaji mimba unahesabika kuwa kosa kubwa, tena ni dhambi [kubwa] inayohitaji toba na msamaha wa Mungu. Katika hali ya kushamiri kwa vitendo vya utoaji mimba, dhana na dhambi itokanayo na vitendo vibaya ya mauaji hupotea, ni kama vile haipo tena. Na serikali zinapotunga sheria za kuwaua watoto wake, hufanya hivyo kwa hasara sio tu yake yenyewe, bali hasa kwa imani ya watu wake. Ukengeushaji mkubwa kati ya imani na tabia za watu hushamirisha watu wenye ubutu wa dhamiri. Upendo hutoweka katika jamii na chuki huchukua nafasi kubwa. Watu wanaishi kwa kutoaminiana, kwa vile hatujui nini kitatokea kwa mwingine.
Utoaji mimba unaua mamilioni ya watu. Miongoni mwao wamo maraisi, mawaziri, wanasayansi, mabingwa wa tiba, walimu na wakulima. Kwa hiyo utoaji mimba unasababisha kuwakosa watu ambao wangetoa mchango mkubwa katika maendeleo ya nchi, kama vile mabingwa wa madawa ya magonjwa mbalimbali. Katika ibada moja ya Dominika, padre akihubiri kuhusu janga la ukimwi, aliwaeleza waamini kisa cha watu kumlilia Mungu ili amalize janga hilo. Lakini Mungu aliwajibu watu, “nimewaletea wataalamu wengi wenye kuelewa tiba ya ukimwi, lakini nyinyi mmewaua kwa utoaji mimba. Kwa hiyo janga hilo la ukimwi litaendelea kuwamaliza kwa kadiri mnavyoendelea kuwaua kwa njia ya utoaji mimba wataalamu ninaowaletea”. Mungu anataka kutuambia kuwa, vitendo vya utoaji mimba vikikoma, basi tutawapata wataamu wenye kujua dawa ya kutibu ukimwi. Tutafakari na tuchukue hatua. Tunawakosa pia vijana ambao wangelitumikia taifa kama wanajeshi, tunawakosa vijana kwa miito ya ukasisi na utawa. Na utamaduni wa utoaji mimba unaposhamiri tunashuhudia kufa kwa imani. Hali hii inajidhihirisha katika kupungua kwa idadi ya waamini katika nyumba za ibada.
Kupungua kwa idadi washirika katika nyumba za ibada ni kiashirio cha kupungua kwa idadi ya watu katika nchi nzima. Idadi ya watu inapopungua, tunakosa nguvu kazi katika uzalishaji, tunakosa soko kwa mazao yanayozalishwa, tunakosa uwekezaji katika mabenki kwa sababu wateja wanapungua, tunakosa watoto wa kujaza shule zetu na hivyo shule nyingi kufungwa. Kwa jumla wake, utoaji mimba unasababisha balaa na laana katika maisha ya jamii. Kubwa zaidi katika laana hizo ni watu kuasi imani yao. Vitendo vya utoaji mimba ni vya kishetani, wakati Mungu anaumba uhai, Shetani anaondoa uhai. Mauti na uzima vinakinzana. Mtu anachagua au uzima ama mauti. Kwa vile kushamiri kwa vitendo vya utoaji mimba ni kiashiria cha kushamiri kwa mauti katika nchi, basi, mauti ikitawala, uzima hutoweka. Nyumba za ibada haziwezi kujaa kwa sababu waamini wake wamegeukia na kuitii mauti. Kwa hiyo utoaji mimba huleta laana kwa taifa na imani zote.